Kesi kati ya AAA & ORS na Kampuni za Uchimbaji was Almasi za Petra Diamonds Ltd Williamson Diamonds Ltd
Makubaliano ya fidia kutoka kwa kampuni ya Petra Diamonds Limited kufuatia unyantasaji wa haki za binadamu
Posted on 12 May 2021
Mkataba wa Makubaliano:
Makubaliano yamefikiwa kati ya Petra Diamonds
Limited na watetezi wa walioyaadhirika, kufuatana na madai makali ya unyanyasaji wa haki za binadamu katika mgodi wa Williamson nchini Tanzania, uliyomilikiwa na asili mia kubwa ya wamiliki binafsi.
Kampuni ya Leigh Day ambayo inawatetea wale wadai 71, imekubali mpango huu wa fidia kwa niaba yao, kulingana na jinsi walivyo jeruhiwa na kutendewa unyanyasaji wa haki zao za bindadamu kutokana na matendo ya walinzi wa mgodi, au au wafanyikazi wa Williamson Diamonds Mine, au Polisi wanaofanya kazi katika mazingara, au katika mgodi wa Williamson Diamond Mine. Kampuni ya Petra Diamonds Limited imekanusha madai haya ikisisitiza ya kwamba haikuwa na uhusiano wowote na wafanyi kazi wa Williamson Diamonds Limited.
Kumi kati ya mashtaka yaliyofichuliwa, yameletwa kutoka jamii za watu waliyosemekana kuwa waliuuawa kupitia kwa matendo yalityofanyika kwa migodi.
Madai haya yaliyopelekwa mbele ya koti kuu ilioko katika mji wa London, Uingereza dhidi ya kampuni ya Petra Diamonds Limited, amabyo in kampuni ya tanzu ya Willimson Diamonds Limited, ilioyomo nchini Tanzania. Kampuni hii imemilikishwa na watu binafsi.
Matekelezo haya yalifanyika miezi ya Februari na Julai mwaka wa 2020.
Kufuatilia mawasiliano ya fanaka kati ya makundi yale mawili, makubaliano
yatajumuisha hatua kadhaa zenye umuhimu mkubwa, ambazo zitafaidisha
waadhirika pamoja na jamii zao kwa jumla, zilizopatikana katika mazingara ya mgod
Mkataba wa makubaliano itajumuisha mapendekezo yafwatayo:
Malipo:
Kampuni ya Petra imekubali kutoa malipo ya kifedha kwa kila mmojawapo wa wale waadhirika 71. Idadi ya pesa atakayopewa kila mdai imeweka katika hali ya siri. Waathirika watapokea Mafunzo ya jinzi ya kulinda pesa zao, na hali kadhalika, watapewa msaada wa jinsi ya kupokea matibabu halisi.
Miradi mbali mbali ya jamaa.
Mfuko wa fedha ya kutekeleza hatua kadhaa ambazo zitatumika kurejesha haki za kisheria kwa wote.
Pia, fedha hizi zitatumika kuendeleza miradi ya kuongeza uchumi kwa jamaa
walioyoishi karibu na mgodi wa Williamson Diamond Mine kwa muda wa miaka mitatu. Miradi hii itachaguliwa kufuatilia mazungumzo na mwelekezo wa jamaa. Miradi itajumuisha mradi mmoja wa kisanii wa uchimbaji wa madini, pamoja na mradi mwingine utakaohusu mpango kwa kubuni biashara ya
ukulima. Thamana ya mfuko wa fedha itaongezwa kwa pesa zilizoko tayari na ambazo tayari zimewekwa kando kwa, madhumuni ya kutekeleza wajibu wa kijamii wa kampuni.
Mradi wa usaidizi wa matibabu:
Kampuni ya Petra itabunisha mradi wa kutoa usaidizi wa matibabu ili uweze kufaidisha jamii kwa jumla. Walakini, lengo kuu la mradi huu litakuwa kuwasaidia walioathirika kupitia ukiukwaji wa haki za binadamu. Mradi wa usaidizi wa matibabu utajumuisha huduma za matibabu na ukarabati pamoja na huduma za kisaikolojia na pia miradi itakayo tumika kuwafikia wengi walio mbali.
Huduma zilizo nje ya vituo vya matibabu zitashirikiana na mahospitali ili iweze kuleta misaada hii na matibabuhaya karibu na jamii vijijini.
Kukubaliwa kutembea kwa migodi:
Hatua wazi na kamilifu zitatekelezwa ili kuwezesha wakazi wa eneleo la mgodi kuingia kwa nia ya kutema kuni na kuchunga au kulisha mifugo yao.
Madai Zaidi:
Itakubalika kwamba ukuchunguzi zaidi wa madai 25 zaidi. Madai haya mapya yataongezwa kwenye kikundi cha madai kilicho tayari kinachuguzwa. Mfumo mkubwa wa kutekeleza uchunguzi wa idadi ya madai haya umekwisha kubaliwa kama mojawapo ya vipimo vya makubaliano.
Utaratibu wa kufuatilia malalamiko ya uendeshaji wa kazi:
Utaratibu ulio kando na majidiliano ya kesi, umekubalika na kukamilika. Nia yake ni kuanza matekelezo yake ya unchunguzi hivi karibuni na katika muda usiyopitisha mwaka mmoja. Utaratibu huu wa katiba utazingatia kanuni na maongozo ya Umoja wa Mataifa kuhusu kazi na haki za binadamu. Lengo la Fumo hili ni kuchunguza kwa kasi, na kutatua madai ya majeraha ya mwili, unyanyasaji wa kijinsia, vifungo visivyo vya haki, na aina zingine za unyanyasaji wa haki za binadamu uliofanyika katika mgodi wa Williamson. Utaratibu unatarajia kuchunguza madai yote kwa kasi, kwa uhaki na kwa uwazi. Pia machungizi yote yatafanyika katika eneo la mgodi. Kila nusu mwaka, kitengo cha ufuatiliaji kisichohusiana na utarabu huu, kita chumbuza maendeleo ya michakato ya Utaratibu wa Kufuatilia malalamiko yote. Ikiwa Utaratibu huu utakosa kufuatilia maendekezo vilivyo kubaiana, Kampuni ya Leigh Day, inashikilia mamlaka yake ya kutetea wale wote ambao wana malalamiko yah alali.
Ruhusa ya kupata recodi ya hospitali:
Katika roho ya kuwa wazi na wa ushirikiano, kampuni zinzaohusika na mashtaka haya, zote zitafichua rekodi na ripoti, pamoja na rekodi kutoka hospitali ya Mwadui, kwa wadai na mawakili wao.
Sera ya watetezi ya haki za binadamu
Pia, kampuni zote zimekubali kubuni sera itakayoamilisha hali za kutonyanyasa na kutesa watu, hivi kwamba sera hizi zitatumika kwa kuwalinda waathirika pamoja na watetezi dhidi ya matendo mengine yatakayosababisha madhara zaidi. Sear hii itatekelezwa hivi karibuni na kwa muda usiyopita miezi miwili.
Kampuni ya Leigh Day imeelewa ya kwamba Petra itatoa taarifa kwa umma ya kueleza jinsi wakosaji wataajibika mbele ya vitendo walivyofanya vya unyanyasaji na uharibifu. Pia, Petra itaonyesha jinsi itaendelea kuhusiana kwa karibu pamoja na taasisi zinazoendesha mashtaka. Zaidi ya hayo, Petra pia itaeleza hatua ambazo itakamilisha kwa jukumu la kuboresha ufuatiliaji na uwabikaji wa vikosi vyake vya ulinzi na usalama katika siku za usoni.
Kampuni ya Leigh Day ingependa kuheshimu waathirika walioleta mashtaka haya wazi wazi. Kwa ajili ya ujasiri huu wao, na azimio lao la kutafuta haki, kesi kimeweza kupata matokeo ya fanaka.
Vile vile, tungependa kuwatambua washirika wenzetu walio Tanzania. Walijitolea kwa kazi hii na walitumia ujuzi pamoja na uvumilivu katika machakato ya unchunguzi. Kati ya washirika hawa waliofanya kazi hii kubwa sana walikuwa viongozi wa jamii, na watetezi wa haki za binadamu walio wasaidia wadai hali kadhalika jamii zilizopatikana katika eneo la Shinyanga.
Vivyo hivyo, tungependa kuta shukrani zetu na kutambua kazi nzuri iliofanywa na wataalamu kutoka nidhamu mbalimbali Pamoja na madaktari na wataalamu watanzania wa kisheria ambao walitekeleza mashauri ya hali ya juu zaidi. Kazi ilyofanywa namashirika ya RAID (Rights and Accountability in Development – Haki na maendelezo ya uwajibikaji) na IPIS (The International Peace Information Service- Shirika la mataifa la Jukumu la Kufuatilisha amani) ilifaulu kwa kuhadharisha na kudhulisha Habari za mashtaka ya ukiukwaji wa haki za binadamu katika mgodi, na pia kwa kuweza kuthibitisha jinsi ya kurejesha malipo ya waathiriwa.
Daniel Leader, mshirika katika Leigh Day alisema kwamba:
Mpango huu wa makubaliano ni mkamilifu na umeweza kuwapa waathiriwa wa unyanyasaji wa haki za binadamu Pamoja na jamaa iliyozingira eneo hili, usaidizi wa hali ya juu. Wafanyikazi wa utaratibu wa kufuatilia malalamiko ya uendeshaji wa kazi pia watatoa usaidizi zaidi na kufuatilia wadai wengine ambao wamejeruhiwa au ambao wana mashtaka yanaoambatana na ukiukwaji wa haki za binadamu. Tutaendelea kufuatilia utekelzaji wa taratibu hii. Tunatarajia pia ya kwamba Petra itaheshimu ahadi yake yote kuhusu makubaliano na vile vile malipo yaliokubaliwa.
Matthew Renshaw, wakili wa wadai katika kampuni ya Leigh Day, alisema kwamba:
Wateja wetu wamefurahisha na matokeo haya. Tunakegemea ya kwamba makubaliano haya yatafaidisha wakaji wa vijiji vilivyozingira mgodi wa Willaimson (Williamson Mine). Ningependa kutambua na kusifu wataalamu wakisheria Pamoja na wataalamu wa matibabu nchini Tanzania, kwa uhodari wao, na kwa mawaidha ya ushauri bora waliotunyunyuzia wakati wa utekelezi huu.
Kwa kweli tunatumaini ya kwamba makubaliano haya pamoja na malipo yataboresha hali ya Maisha na kuleta tofauti kwa thamani ya afya kwa maisha ya watu wengi katika miaka ijayo.